Ruhusu kwa wanandoa kufanya jimaa mchana wa Ramadhaan safarini

Swali: Kuna mwanamume ambaye alikuwa si mwenye kufunga katika Ramadhaan. Hiyo ilikuwa ni kwa sababu ya safari yake kutoka Twaaif kwenda Tabuuk ambapo alikuwa yeye na mke wake. Wote wawili walikuwa si wenye kufunga. Mwanamume huyo akamwingilia mke wake mchana wa Ramadhaan. Je, mwanamume analazimika kutoa kafara au anatakiwa kulipa siku hiyo tu? Mke ana nini ikiwa aliridhia au hakuridhia jimaa hiyo?

Jibu: Mambo yakiwa kama ulivyotaja na kwamba jimaa ilitokea safarini, hakuna jengine linalomlazimu mume wala mke isipokuwa kulipa siku hiyo tu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/316)
  • Imechapishwa: 17/06/2017