Ruhusa ya mke juu ya kufunga swawm ya nadhiri na kafara

Swali: Je, mke amuombe ruhusa mume wake katika swawm ya nadhiri?

Jibu: Swawm ya nadhiri na kafara zinatakiwa kuangaliwa vizuri; ikiwa ni swawm ambayo haikufungamanishwa (مطلقًا), basi anaweza kuichelewesha na ikiwa ameifungamanisha basi anatakiwa kuiharakisha na inaungana na swawm ya faradhi. Kuifungamanisha ni kulenga kufunga siku maalum au mwezi maalum. Kwa sababu ni faradhi. Lakini ikiwa haikufungamanishwa anaruhusiwa kuichelewesha mpaka wakati fulani.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21656/هل-تستاذن-المراة-زوجها-في-صوم-النذر
  • Imechapishwa: 05/09/2022