Swali: Mtu ambaye shaytwaan amemshawishi na akamwendea mwanamke ambaye ni ajinabi na akafanya nae mapenzi bila ya jimaa kitendo hicho kitahitajia adhabu kama adhabu ya kufanya zinaa au inatosha kuomba msamaha?

Jibu: Tawbah na kuomba msamaha kunatosheleza. Vilevile ahifadhi swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijiwa na mtu ambaye alikuwa amefanya kila kitu na mwanamke mmoja isipokuwa jimaa tu, mtu huyu akaja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumuuliza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakaa kimywa mpaka kulipoteremsha Kauli Yake (Ta´ala):

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ

“Na simamisha swalah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku, hakika mazuri yanaondosha mabaya. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.” (11:114)

Mtu yule akamuuliza: “Ee Mtume wa Allaah! Aayah hii inanihusu mimi peke yangu au watu wote?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajibu na kusema:

“Ni kwa watu wote.”

Mwenye kuhifadhi swalah za faradhi, Allaah kwa swalah hizo anamsamehe madhambi madogo madogo – himdi zote anastahiki Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13382
  • Imechapishwa: 27/04/2018