Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke yeyote kumwomba mume wake talaka bila ya sababu ya msingi, basi ni haramu juu yaka harufu ya Pepo.”

Mume wake anakula ribaa na anafanya baadhi ya haramu. Je, haya yanamjuzishia kuomba talaka?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… bila ya sababu ya msingi.”

Kuomba kwake talaka kuna msingi. Anakula ribaa na anafanya nayo biashara. Kuna sababu ya msingi. Aombe talaka kutoka kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (103) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-6-3-1441_1.mp3
  • Imechapishwa: 09/01/2021