Rekodi za video ni mbaya zaidi kuliko picha za kivuli


Naona kuwa rekodi za video ni mbaya zaidi kuliko picha za kivuli. Kwa nini? Kwa sababu hoja zetu dhidi ya wale wanaokwenda kinyume ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale wanaoigiliza uumbaji wa Allaah.”

Yule anayechora uumbaji wa Allaah (´Azza wa Jall) anaigiliza uumbaji Wake, pasi na kujali ni njia au kifaa gani ametumia. Allaah (´Azza wa Jall) ameharamisha juu ya viumbe Wake kumwigiliza kwa picha. Je, kalamu na manyoya zinafanya picha sahihi zaidi kuliko kamera? Hapana shaka kwamba kamera ndio yenye kufanya sahihi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (834) Dakika: 44:18
  • Imechapishwa: 01/07/2021