Swali: Kuna rangi ya nywele ambayo yenyewe si nyeusi, lakini inapowekwa kwenye nywele nyeupe basi nywele zinageuka kuwa nyeusi. Je, inajuzu kuzipaka nywele rangi hii?

Jibu: Midhali ikiwekwa kwenye nywele hizi nyeupe zinageuka kuwa nyeusi basi ni haramu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuzigeuza mvi kwa rangi nyingine lakini akakataza rangi nyeusi pale aliposema:

“Jiepusheni na rangi nyeusi.”

Kumepokelewa vilevile matishi makali kwa mtu ambaye anapaka rangi nyeusi. Hivyo ni wajibu kwa mtu kumcha Allaah (´Azza wa Jall). Hata kama  nywele zake ni nyeupe bado anazingatiwa ni kijana midhali ni mwenye uchangamfu na ni mwenye nguvu. Na hata kama atakuwa na nywele nyeusi lakini akawa ni dhaifu na myongenyonge anazingatiwa kuwa ni mzee.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (59) http://binothaimeen.net/content/1353
  • Imechapishwa: 23/11/2019