Swali: Kuna mgonjwa mwenye maradhi ya kisukari ambaye hakuweza kufunga Ramadhaan. Baada ya Ramadhaan akahisi nafuu na akaona kuwa analazimika kulipa Ramadhaan. Alijaribu siku moja na akashinda taabani. Maradhi haya yuko nayo siku nyingi. Ni ipi hukumu yake?

Jibu: Huyu anatakiwa kulisha kwa kila siku moja masikini. Kwa sababu aliacha kufunga kwa maradhi yasiyotarajiwa kupona. Maradhi ya kisukari – Allaah atulinde sisi na nyinyi – mara nyingi hayaponi. Kwa hivyo anatakiwa kulisha kwa kila siku moja masikini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/115)
  • Imechapishwa: 18/06/2017