Swali: Mwanamke amepatwa na kiharusi na madaktari wamemkataza kufunga. Ni ipi hukumu?

Jibu: Allaah (Ta´ala) amesema:

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

“Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo la batili. Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge. Atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyinginezo. Allaah anakutakieni mepesi – na wala hakutakieni magumu. Na ili mkamilishe idadi [katika wakati wake uliyowekwa] na ili mumtukuze Allaah kwa kuwa amekuongozeni na ili mpate kushukuru.”[1]

Mtu akiwa na ugonjwa ambao hautarajiwi kupona basi anatakiwa kulisha kwa kila siku moja masikini. Namna ya kutoa ni kuwagawia chakula kama vile mchele. Imependekezwa vilevile kuwapa kitoweo kama vile nyama au kitu kingine. Anaweza vilevike kuwaalika masikini katika chakula cha jioni au chakula cha mchana na akawalisha. Hii ndio hukumu ya mgonjwa mwenye maradhi yasiyotarajiwa kupona. Mwanamke huyu aliyepatwa na maradhi haya yaliyotajwa na muulizaji anaingia katika aina ya wagonjwa hawa. Ni wajibu kwake kulisha kwa kila siku moja masikini.

[1] 02:185

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/115)
  • Imechapishwa: 18/06/2017