Swali: Kuna mgonjwa ana ugonjwa wa figo na hawezi kufunga kwa sababu daktari amemnasihi kutumia maji kila wakati. Amemwambia vilevile kuwa kufunga kunamzidishia kuugua zaidi na kutapelekea kuliharibu kabisa. Ni ipi hukumu?

Jibu: Haya yanazingatiwa ni maradhi kweli na inavyoonekana yanahesabika ni katika maradhi yenye kuendelea. Ni wajibu kwake kulisha kwa kila siku moja masikini kama tulivyotangulia kusema. Namna ya kutoa chakula ima anaweza kupika chakula na akawaalika masikini ili wale katika chakula hiyo au amtengee mchele, ngano na n.k. na kumpa kila masikini mmoja. Akimwongezea vilevile kwa kumpa kitoweo kama nyama au kitu kingine basi atakuwa amefanya vizuri na bora zaidi.

Lakini ikiwa daktari atamwambia kwamba kufunga pamoja na maradhi haya kunamdhuru wakati wa majira ya joto na kwamba hayamdhuru wakati wa majira ya baridi, basi acheleweshe swawm mpaka wakati wa majira ya baridi. Katika hali hiyo hatotakiwa kulisha. Huyu hali yake inatofautiana na ya yule ambaye kufunga kunamdhuru siku zote. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/124-125)
  • Imechapishwa: 19/06/2017