Ramadhaan na maradhi ya kubadilishwa moyo

Swali: Miaka saba iliopita nimefanyiwa operesheni ya kuondolewa moyo na kubadilishiwa moyo mwingine ambapo operesheni imefaulu na himdi zote njema anastahiki Allaah. Mosi: Nakuombea uniombee du´aa na ndugu wahudhuriaji waitikie “Aamiyn” kwamba kufaulu huku kuendelee, Allaah aniwafikishe kunyooka na kushukuru juu ya neema hii.

Pili: Daktari na msimamizi wangu ambaye anafuatilia hali yangu amenishauri kwamba sintoweza kufunga swawm ya mwezi wa Ramadhaan inayokaribia. Ni ipi hukumu pamoja na kuzingatia kwamba sio katika Ahl-us-Sunnah? Jambo la mwisho nifanye nini juu ya masiku ninayodaiwa ya Ramadhaan iliopita niliyokula wakati hali yangu ilikuwa yenye kudhoofika?

Jibu: Namuomba Allaah (Ta´ala) aidumishe shifaa yake na amfanye kuwa imara katika dini ya Allaah. Hii ni neema ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) juu yake. Atumie fursa ya kufanya ´ibaadah kwa wingi katika kusema “Subhaan Allaah”, “Allaahu Akbar,” “Laa ilaaha illa Allaah”,  kusoma Qur-aan, kutoa swadaqah akiwa ni mwenye pesa na zenye kufanana na hizo.

Ama kuhusu swawm asifunge. Daktari mwaminifu akimwambia kwamba kufunga huenda ikawa ni sababu ya maradhi kurudi, basi hapo itakuwa ni haramu kwake kufunga. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا

“Wala msiziue nafsi zenu. Hakika Allaah ni Mwenye kuwahurumia.”[1]

Asubiri mpaka pale Allaah atapomponyesha uponaji wa kikamilifu na daktari wake akampa idhini ya kufunga.

Kuhusu siku zilizompita akipona uponaji wa kikamilifu basi azilipe pamoja na Ramadhaan inayokaribia.

[1] 04:29

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1573
  • Imechapishwa: 09/03/2020