Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefunga Ramadhaan kwa imani na matarajio, basi atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”

Je, madhambi haya kunaingia pia madhambi makubwa?

Jibu: Hapa wanachuoni wametofautiana. Maoni sahihi ni kwamba hayahusiana na madhambi makubwa. Ni lazima mtu atubie juu ya madhambi makubwa. Inahusiana na madhambi madogo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah tano, ijumaa mpaka ijumaa nyingine, Ramadhaan mpaka Ramadhaan nyingine vinafuta yale yaliyo baina yake midhali mtu atajiepusha madhambi makubwa.”

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ

“Mkijiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa, basi Tutakufutieni madhambi yenu madogo.” (04:31)

Kilicho wazi katika dalili ni kwamba kusamehewa kunakuwa katika madhambi madogo. Madhambi madogo ndio ambayo yanafutwa kwa kutenda matendo mema. Kuhusu madhambi makubwa ni lazima mtu atubie.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 06/06/2017