Rak´ah mbili za wudhuu´ kuziswali wakati uliyokatazwa

Swali: Kwa kutegemea Hadiyth ya Bilaal (Radhiya Allaahu ´anh):

“Sikupatapo kutawadha isipokuwa niliswali Rak´ah mbili baada ya wudhuu´.”

Mimi baadhi ya nyakati natawadha wakati uliokatazwa kuswali ndani yake. Mfano wa hilo ni baada ya swalah ya ´Aswr, baada ya swalah ya Fajr au wakati wa kuzama kwa jua na wakati wa kuchomoza kwake. Je, ninapata dhambi nikiswali Rak´ah mbili za wudhuu´?

Jibu: Kilichopendekezwa ni wudhuu´. Kilichopendekezwa ni mtu kutawadha na kuswali Rak´ah mbili ambazo ni Sunnah ya wudhuu´ katika wakati wowote hata kama ni wakati uliokatazwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kutawadha mfano wa wudhuu´ wangu huu kisha akaswali Rak´ah mbili na asiizungumzishe nafsi yake kati ya mawili hayo, basi Allaah atamsamehe dhambi zake zilizotangulia.”

Kinacholengwa ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitawadha basi anaswali Rak´ah mbili na akawakokoteza watu kufanya hivo. Zinaitwa “Sunnat-ul-Wudhuu´”. Hakuna neno kuziswali wakati uliokatazwa na wakati mwingineo. Kwa sababu ni Sunnah iliyokokotezwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9505/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B1%D9%83%D8%B9%D8%AA%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%88%D8%B6%D9%88%D8%A1-%D9%88%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%AA%D9%87%D8%A7-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%88%D9%82%D8%A7%D8%AA-%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%87%D9%8A
  • Imechapishwa: 21/02/2020