Swali: Kuna watu wawili. Mmoja wao haswali kabisa, mwingine haswali swalah kwa mkusanyiko lakini anadai kwamba anaswali nyumbani kwake. Je, inajuzu kuzungumza, kula, kunywa na kucheka pamoja nao?

Jibu: Ambaye haswali kabisa ni kafiri na mwenye kuritadi. Huyu ni mbaya zaidi kuliko mayahudi na manaswara. Myahudi na mnaswara anaweza kuendelea kushikilia dini yake tofauti na mtu ambaye haswali.

Yule asiyeswali pamoja na mkusanyiko ni mtenda dhambi, lakini sio kafiri.

Haijuzu kwa mtu kufanya urafiki na makafiri na watenda madhambi kwa njia ya kwamba akatafuta mapenzi kutoka kwao. Hata hivyo inafaa kwake akala na kucheka nao akiwa na matarajio ya wao kuongoka. Tunatambua sote namna ilivyo muhimu kuwafanya watu wakavutiwa na Uislamu. Kwa ajili hiyo zakaah, ambayo ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu, inafaa kuwapa nayo makafiri kwa lengo la kuwapendezea na kuwavutia Uislamu.

Kwa msemo mwingine, ikiwa mtu anatarajia kutoka kwa mtu asiyeswali pamoja na mkusanyiko au ambaye haswali kabisa kwamba ataongoka iwapo atacheka nao, akanywa na kula nao, basi mtu afanye hivo. Lakini mtu akiwa hatarajii hilo, basi asifanye. Lakini hilo halizuii kuwanasihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (19 B) Dakika: 15:42
  • Imechapishwa: 21/06/2021