Swali: Kuna watu wanaotumia hoja kujuzisha maandamano kwa waislamu kukusanyika kwenye Ka´bah baada ya ´Umar na Hamzah kuingia katika Uislamu, pia mtu ambaye aliweka samani nje ya nyumba yake ili watu wajue ubaya wa jirani yake…

Jibu: Kisa cha ´Umar na Hamzah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) waliposilimu wakatoka kwenye Masjid al-Haram. Je, haya ni maandamano kwa watu gani? Ni kwa makafiri na si kwa waislamu. Haya ni maandamano kwa makafiri na si kwa waislamu. Maandamano kwa waislamu hayajuzu.

Jambo la pili ni kuwa upokezi huu unasemekana haikuthibiti. Lakini tukisema imethibiti, hawakuandamana maandamano. Wao walitoka kwa ajili ya swalah. Hawakuandamana, hawakupiga kelele, fujo n.k. Hawakufanya haya. Walitoka nje tu kwa ajili ya Swalah.

Je, kuna yeyote anayekukataza kutoka kwenye Masjid al-Haram? Walitoka kwa pamoja ili waswali kwenye Masjid al-Haram. Kwa hivyo sio dalili ya maandamano.

Ama mtu kutoa samani yake ni kwa ajili watu wajue kuwa jirani yake anamuudhi. Haya sio maandamano. Ni alama ya hasira za jirani. Sio maandamano. Je, ni maandamano kutoa nje vyombo vya jikoni na samani – je haya ndiyo maanamdano?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13267
  • Imechapishwa: 05/09/2020