Radd kwa ambaye anaona kuwa inafaa kutufu kwenye makaburi

Swali: Ni ipi Radd bora kwa yule ambaye anaona kuwa inafaa kutufu kwenye makaburi?

Jibu: Radd kwake ni kwamba kitendo hichi ni katika Bid´ah. Akitufu juu ya yule mtu anakuwa mshirikika na mwenye kuritadi. Kwa sababu Twawaaf ni ´ibaadah. Mwenye kumtekelezea ´ibaadah asiyekuwa Allaah anakuwa mshirikina. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Sikuumba majini na watu isipokuwa waniabudu.” (51:56)

Amewaumba viumbe kwa ajili ya ´ibaadah. Akimwabudu asiyekuwa Allaah ameshirikisha. Akitufu kwenye kaburi hali ya kujikurubisha kwalo, akaliomba, akalichinjia, akaliwekea nadhiri, akaswali, akarukuu au akasujudu kwa ajili yake anakuwa amemwabudu asiyekuwa Allaah na anakuwa mshirika.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 19/10/2018