Swali: Leo tunasikia watu wenye kuita kwenye kuwa na uhuru wa ´Aqiydah na wanatumia dalili ya hili kwa Kauli Yake (Ta´ala):

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ

“Hapana kulazimisha katika Dini.” (02:256)

أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ

“Je, basi wewe utashurutisha watu mpaka wawe Waumini?” (10:99)

Ni ipi hukumu ya madai haya na kuyaeneza kwa Ummah?

Jibu: Tulizungumzia hili kwenye kikao cha kwanza na kusema ya kwamba kuna watu wanaopinga ´Aqiydah na wanasema kuwa inatoshelezwa kuitwa kwa jina la Uislamu na hakuna tofauti kati ya watu wanaojiita kuwa ni Waislamu; hakuna tofauti kati ya mpwekeshaji na mshirikina, mtu wa Sunnah na mtu wa Bid´ah, mtu wa Sunnah na Raafidhwiy na wenye kujinasibisha na Uislamu pasina kujali kundi lao, haya ni madhehebu batili na ni maneno ya batili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah huu utagawanyika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni kina nano hao, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni yule atayekuwa katika yale niliyomo mimi na Maswahabah zangu.”

Hili ni jambo la lazima. Haya ni madai ya batili. Kuhusiana na Kauli Yake (Ta´ala):

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ

“Hapana kulazimisha katika Dini.”

Ni kama mlivyosikia ya kwamba uongofu uko kwa Allaah:

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ

“Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye.”

Sisi hatuwapigi watu vita na kuwalingania kwa kuwalazimisha Dini. Kuiingiza imani ndani ya moyo hakuna anayeweza kufanya hivo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Lakini hata hivyo sisi tumeamrishwa kupigana Jihaad na kulingania katika Dini ya Allaah. Kuhusu kuwaongoza watu na kuiingiza imani kwenye mioyo yao, hili hatulimiliki. Ni jambo linalomilikiwa na Allaah (Jalla wa ´Alaa).

أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ

“Je, basi wewe utashurutisha watu mpaka wawe Waumini?” (10:99)

Ni kama mfano wa Kauli:

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ

“Hapana kulazimisha katika Dini.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hamiliki kuweza kuiweka imani kwenye moyo. Hili liko Mikononi mwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Pamoja na hivyo ameamrishwa kulingania katika Dini ya Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kupigana Jihaad.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_01.mp3
  • Imechapishwa: 03/07/2018