Rabiy´ al-Madkhaliy – Muhaddith na bakora kwa Hizbiyyuun

Swali: Hazzaa´ huyu anamtuhumu Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy ya kwamba ni mtu mwenye papara wakati anapowahukumu watu, hana umakinifu, hakasiriki isipokuwa kwa ajili ya nafsi yake na kwamba anaenda kinyume na mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni vipi unaraddi usengenyaji huu na uongo huu kwa wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah? Tunapenda ututajie baadhi ya matunda mazuri ya Shaykh Rabiy´ juu ya Da´wah ya Salafiyyah ili watu Indonesia waweze kumtambua.

Jibu: Shaykh Rabiy´ anazingatiwa kuwa ni mmoja katika wanachuoni mashuhuri zaidi katika elimu ya Hadiyth na himdi zote zinamstahikia Allaa. Hili ni mosi.

Pili ni Ruduud zake alizowatwanga Hizbiyyuun. Ni kweli ya kwamba amewafanya wakapata maumivu. Hawakupigi makelele isipokuwa kuna jambo. Allaah amjaze kheri na amlipe kwa kutetea kwake Sunnah. Hata hivyo ni mwanaadamu ambaye anapatia na anakosea. Wakati fulani anayajua mambo fulani na wakati mwingine hayajui. Sisi hatumtetei kama wao. Ndugu! Hizbiyyuun wanawaadhimisha, wanarejea na kuwakumbatia watu wao hata kama watakuwa hawana kichwa sawa na kitunguu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=21
  • Imechapishwa: 08/04/2017