Rabiy´ al-Madkhaliy mtazamo wake juu ya Irjaa´ na utatu wa Irjaa´


Tangu mwanzoni mwa maisha yangu kama mwanafunzi, msomeshaji na mtunzi nilisema, kuthibitisha na kumuabudu Allaah kwa kusema:

Imani ni maneno na matendo; matendo ya moyo na ya ulimi na matendo ya viungo. Inapanda kwa matendo mema na inashuka kwa maasi. Wakati fulani naweza kusema kuwa inashuka mpaka hakubaki imani sawa na punje kidogo. Wakati mwingine naweza kusema kuwa inashuka mpaka hakubaki katika imani chochote. Mmoja katika marafiki zangu amekusanya kitabu kuhusu mtazamo wangu juu ya imani. Kitatawanywa katika sahab.net

Kadhalika 1425 nimeandika makala tatu kuhusu tamko “Jins-ul-´Amal”[1]. Ndani yake nimebainisha kwamba wale wanaolitumia wana malengo mane ambapo moja wapo ni kuwatuhumu Ahl-us-Sunnah Irjaa´ na kupachika Irjaa´ ya utatu kwa wanachuoni wa sasa kama vile Ibn Baaz, al-Albaaniy na Ibn ´Uthaymiyn.

[1] Tazama http://wanachuoni.com/content/neno-jins-ul-%C2%B4amal-limetoka-kwa-murji-ah

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 101
  • Imechapishwa: 09/10/2016