Raatibah ya Fajr kwanza au faradhi?

Swali: Mtu akiamka kabla ya kuchomoza kwa jua kwa kipindi ambacho hakitoshi isipokuwa kuswali Rak´ah mbili peke yake ni kipi atangulize; swalah ya faradhi au sunnah ya kabla ya Fajr?

Jibu: Atatakiwa kutanguliza sunnah ya kabla ya Fajr. Ni mwenye kupewa udhuru. Kwa sababu muda wake juu yake unaanza kuanzia ule wakati alipoamka na si kuanzia ule wakati wa kuchomoza kwa jua. Hilo ni kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Yule atakayelala na kupitikiwa na swalah au akaisahau basi aiswali pale atakapokumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”

Kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru.

Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia ilipompita alitawadha kisha akaswali Raatibah halafu ndio akaswali faradhi. Hii ndio dalili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 07/11/2020