Raatibah na Tahiyyat-ul-Masjid kwa nia moja


Swali: Mimi huswali Maghrib ninapokuwa njiani na hutoka moja kwa moja baada ya swalah ili niwahi darsa. Ninapoingia msikitini huswali swalah ya mamkuzi ya msikiti na nikanuia kwa swalah hiyo Sunnah ya Raatibah. Je, nifanyavo ni sawa?

Jibu: Kitendo chako hichi ni sawa. Ni kama ambavo mtu akija na akakuta kumeshakimiwa swalah basi swalah ya faradhi inatosheleza kutokamana na swalah ya mamkuzi ya msikiti.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 16/07/2021