Swali: Tunawasikia Raafidhwah katika adhaana yao wanasema:

“Tunashuhudia ya kwamba ´Aliy ni walii wa Allaah.”

Sisi tunawakemea matamshi haya. Tuwakataze matamko au maana yake?

Jibu: Ambaye anakubali haki katika wao mbainishieni na mwambieni kuwa adhaana ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) iliyothibiti kutoka kwake hakuna matamshi haya. Waambieni kuwa sisi ni wenye kufuata na sio wenye kuzua. Wabainishieni haya. Yule mwenye kukubali ni sawa na asiyekubali hoja itakuwa ni yenye kumsimamia.

Lakini kitu cha kwanza mnatakiwa kuisahihisha ´Aqiydah yao kabla ya adhaana. Wana mambo mbali na hili. Wabainishieni, muwanasihi na muwapambanulie Tawhiyd na ´Aqiydah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnaja.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 18/11/2016