Qur-aan ni maneno ya Allaah na wino na makaratasi ni sanaa yetu

Swali: Je, inajuzu kusema herufi kwenye karatasi za Qur-aan zimeumbwa?

Jibu: Maneno ni ya Allaah. Wino na makaratasi ni sanaa yenu. Uandishi ni wetu. Ndio maana baadhi ya hati zinakuwa nzuri na zingine zinakuwa si nzuri. Ni matendo yetu. Ama kuhusiana na Qur-aan, yote imepangwa na nzuri. Hata hivyo uandishi ni wa kwetu na ni matendo yetu. Wino ni wa kwetu. Makaratasi ni yetu. Pamoja na hivyo kilichoandikwa ni maneno ya Allaah. Kinachosomwa ni maneno ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–02041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015