Qur-aan ina maana ya udhahiri na ya undani?

Swali: Inajuzu kusema kuwa Qur-aan ina maana ya udhahiri na ya undani?

Jibu: Msemo huu kwamba Qur-aan ina maana ya udhahiri na ya undani ni msemo wa wakanamungu (Malaahidah). Wao ndio wanasema kuwa maandiko yote yana maana ya udhahiri na ya undani. Maana ya udhahiri ni ya waislamu na maana ya undani ni ya kwao. Qur-aan ina maana yenye kujulikana na ilio wazi. Hakuna kitu kilichofichikana. Vivyo hivyo Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah (04)
  • Imechapishwa: 30/04/2020