Qunuut katika swalah za mchana za kusoma kimyakimya


Swali: Je, imewekwa katika Shari´ah wakati wa matukio ya majanga imamu kusoma Qunuut katika swalah za kusoma kimyakimya kama katika Dhuhr na ´Aswr? Katika hali hiyo asome kwa sauti?

Jibu: Asome hivo katika kila swalah; swalah za mchana na za usiku.

Swali: Je, asome kwa sauti?

Jibu: Ikiwa wanaswali kwa mkusanyiko asome kwa sauti. Baada ya hapo na wao watasema “Aamiyn”. Hata hivyo mtu ikiwa anaswali peke yake asisome kwa sauti.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (64) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighatsah%2019-03-1438H.mp3%2001.mp3
  • Imechapishwa: 09/10/2017