Qunuut katika swalah za faradhi

Swali: Ni ipi hukumu ya kukunuti katika swalah za faradhi? Ni ipi hukumu kukiwafikia waislamu majanga?

Jibu: Kufanya Qunuut katika swalah za faradhi ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Haitakikani kufanya hivo. Lakini imamu akileta Qunuut mfuate kwa sababu tofauti ni shari.

Waislamu wakifikwa na maafaa basi hapo ni sawa kufanya Qunuut kwa ajili ya kumuomba Allaah (Ta´ala) ayaondoshe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 351
  • Imechapishwa: 31/05/2019