Swali: Wakati fulani tunamuona imamu akikunuti katika Rukuu´ baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´ na si kabla yake. Je, kitendo hichi kinafaa?

Jibu: Ndio. Qunuut inafaa kabla na baada ya Rukuu´. Lakini hata hivyo itambulike kuwa hakuna Qunuut katika swalah. Qunuut inakuwa katika swalah ya usiku. Ama kuhusu swalah za faradhi inafaa wakati waislamu watapopatwa na maafa basi kiongozi, ambaye ni yule raisi wa nchi, ataleta Qunuut. Akunuti pia yule ambaye raisi wa nchi atamwamrisha kufanya hivo. Raisi wa nchi asipoamrisha kusoma Qunuut basi watu wasifanye hivo. Kwa sababu kukunuti wakati wa majanga ni jambo linarudi kwa kiongozi wa nchi na si mtu mmoja mmoja. Kwa dalili kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisoma Qunuut wakati wa majanga na wala hatukuhifadhi kwamba aliwaamrisha watu wa misikiti mingine kufanya hivo. Jambo la kusoma Qunuut wakati wa majanga linarudi kwa kiongozi wa nchi; akiliamrisha basi anatakiwa kutiiwa, na asipoliamrisha watu wasifanye. Du´aa haikukomeka katika Qunuut. Mtu anaweza kumuomba Allaah (Ta´ala) akiwa katika Sujuud, kati ya adhaana na Iqaamah. Kuitikiwa kwa du´aa ni jambo halikukomeka katika du´aa ya Qunuut.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (377) http://binothaimeen.net/content/13365
  • Imechapishwa: 08/10/2020