Qudaamah bin Madh´uun alikuwa ni Abu ´Amr al-Jumhiy. Ni miongoni mwa wale waislamu waliotangulia mwanzo ambao wameshirika vita vya Badr. Alikuwa ni kiongozi wa Bahrayn wakati wa ´Umar. Alikuwa ni mjomba wake mama wa waumini Hafswah na Ibn ´Umar. Alikuwa amemuoa shangazi yao Hafswah bint al-Khattwaab, mmoja katika wanawake waliofanya Hijrah.

Qudaamah alifanya Hijrah kwenda Uhabeshi. Kuna kipindi alikunywa pombe kutokana na kuelewa kimakosa maneno ya Allaah (Ta´ala):

لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا

“Hakuna dhambi juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula [kabla ya kuharimishwa]… “[1]

´Umar akampiga bakora na akamwondoa kutoka Bahrayn.

Ayyuub as-Sikhtiyaaniy amesema:

“Mtu pekee aliyeshiriki vita vya Badr na akapigwa bakora ni yeye.”

Sivyo hivo. Kuna mwingine tena: Nu´aymaan bin ´Amr al-Answaariy an-Najjaariy mfanya mzaha.

Ibn Sa´d amesema:

“Watoto wa Qudaamah alikuwa ´Umar, Faatwimah na ´Âishah. Alifanya Hijrah ya pili kwenda Uhabeshi na alishuhudia vita vya Badr na Uhud.”

´Aaishah bint Qudaamah amesema kuwa baba yake alikufa mwaka wa 36. Aliishi miaka 68. Alikuwa hazipaki rangi mvi zake. Alikuwa mrefu na kahawia. Allaah amuwie radhi.

[1] 5:93

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (1/161-162)
  • Imechapishwa: 18/01/2021