Swali: Vipi kuhusu kuweka Qaswiydah na Anaashiyd kama mlio wa simu?

Jibu: Hii ni mifumo ya Ahl-ul-Bid´ah. Kimsingi Anaashidy hizi za kidini zimetoka kwa Suufiyyah. Usifanye hivo na wala usiziweke katika simu yako. Wakati mwingine Qaswiydah hizi zinakuwa na kitu katika Adhkaar na khaswa zile Qaswiydah wanazoita kuwa ni za dini au za Zuhd ambazo zinazosisitiza juu ya Aakhirah na kuipa nyongo dunia. Kunaweza kuwa kuna kipande ambacho kinamtaja Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) au kinachotaja jina la Allaah. Hili si sawa. Haijuzu kuweka kitu katika haya.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://miraath.net/ar/content/fatawa/8883520
  • Imechapishwa: 26/11/2017