Swali: Kuna kijana amejitoa manii mchana wa Ramadhaan. Ni lipi la wajibu kwake?

Jibu: Punyeto mchana wa Ramadhaan inaharibu swawm ikiwa mtu atakusudia kufanya hivo na akatokwa na manii. Ni lazima kwake kulipa ikiwa swawm yake ni ya faradhi. Ni lazima vilevile kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa sababu kujitoa manii haijuzu sawa katika hali ya funga na hali isiyokuwa ya funga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/267)
  • Imechapishwa: 27/05/2018