Swali: Je, inajuzu kwa mtu akichelea kutumbukia katika uzinzi badala yake ajichue sehemu ya siri?

Jibu: Hapana, haijuzu. Afunge. Atumie swawm, kama alivyoelekeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Msafiri akitua njiani kwa muda wa siku moja akusanye kati ya swalah pamoja na kwamba anasikia adhaana?

Jibu: Kufaa inafaa midhali yeye ni msafiri. Lakini lililo bora ikiwa msikiti uko karibu basi aende na kuswali pamoja na waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (22) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdatul-26-3-1435.mp3
  • Imechapishwa: 29/03/2020