Punde tu baada ya mazishi


Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Liharakisheni jeneza. Akiwa mwema, basi ni kheri mnayomtangulizia, na akiwa kinyume na hivo, basi hiyo ni shari mnayoiondoa kutoka kwenye shingo zenu.”[1]

Hadiyth inafahamisha pia kwamba maisha ya ndani ya kaburi yanayo neema na adhabu, jambo ambalo kumepokelewa juu yake lukuki ya Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwanzoni mwa maisha yao ni pale tu ambapo mtu atazikwa ndani ya kaburi lake. Ndio maana ikawa ni jambo lililowekwa katika Shari´ah punde tu baada ya mazishi mtu akasimama karibu na kaburi lake, akamwombea du´aa, msamaha na thabati kwa Allaah.

[1] al-Bukhaariy (1315) na Muslim (944).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjat-ul-Abraar, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 27/02/2021