Pumzi Za Mwisho Kabla Ya Kukata Roho


Swali: Baadhi yao wanasema kuwa fitina hii ndio bado imeanza sasa. Tuwajibu vipi?

Jibu: Ndio, fitina hii ndio bado imeanza kwa Hajaawirah na Ma´aabirah. Jina “Ma´aabirah” halikutoka kwetu, limetoka Libya. Hivyo ndivyo wanavowaita wafuasi wa Abul-Hasan. Fitina hizi mbili kwa wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah zimeisha na zimekuwa wazi. Ni za zamani na zilizokatika, pofu, ziwi, bubu, kilema na mapengu. Wanajikongoja tu kwa zile pumzi za mwishoni mwishoni kabla ya kufa. Tumemalizana nao na himdi zote ni za Allaah. Subira mwisho wake ni mzuri. Tulimvumilia al-Hajuuriy, kama alivyosema Shaykh Rabiy´, miaka saba kama si zaidi. Kosa lake likazidi kudhihiri zaidi jinsi muda unavyokwenda.

Aliyemnasihi Abul-Hasan akamraddi. Hamuheshimu mwanachuoni, mzee, kijana, mwanafunzi, makundi wala yeyote. Masikini Ahl-us-Sunnah waliomnasihi. Hali kadhalika al-Hajuuriy. Masikini waliomnasihi. Hajali si wewe, kijana, mwanachuoni, mlinganizi, mwanafunzi, anayempenda au anayemjali. Ole wako ikiwa humsapoti. Hatukujifunza hilo katika mfumo wa Salaf; kuwa na mizozo na wanachuoni. Kamwe hatukutambua kitu kama hicho. Hayo yanapatikana tu kwa al-Hajuuriy na Abul-Hasan. Da´wah yetu imejengwa juu ya adabu. Ikiwa tunamheshimu mwanafunzi, tusemeje juu ya mwanachuoni? Ambaye si msomi akija na kukupa nasaha, kukutajia faida au suala, tunamuombea kwa Allaah amjaze kheri na kumshukuru. Hatukufikiri hilo. Mwanaadamu ni dhaifu. Sisi sio Malaika. Namna hiyo ndivyo tunavyotaamiliana na mwanafunzi; vipi tusemeje inapokuja kwa mwanachuoni mwenye cheo cha chini, cha kati na kati, seuze mwenye cheo cha juu? Midhali anasema kweli tunamuomba Allaah amjaze kheri kwa uzinduzi na ukumbushaji.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wusswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2865
  • Imechapishwa: 18/01/2017