Swali: Hii leo watu wanatawanya nyujumbe kati ya watu kwa njia ya simu zinazoharamisha kupeana hongera siku moja au mbili kabla ya kuanza kwa sikukuu ya ´iyd na kwamba kitendo hicho ni katika Bid´ah. Unasemaje?

Jibu: Sijui kuhusu maneno haya. Ni mambo wanayoyatawanya na sijui kuwa yana msingi wowote. Kupeana hongera ni kitu kinachofaa ile siku ya ´iyd na baada ya siku ya ´iyd. Ni kitu kinachofaa. Ama kupeana hongera kabla ya siku ya ´iyd ni kitu sijui kuwa Salaf walikifanya kwamba walipeana hongera kabla ya kuanza siku ya ´iyd. Ni vipi watapeana hongera kwa kitu ambacho hakijaanza? Kupeana hongera kunakuwa ile siku ya ´iyd au baada ya siku ya ´iyd. Ingawa pia hakuna dalili juu ya hilo. Lakini Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema kuwa yeye haanzi kumpa mtu hongera. Lakini kwamba anamwitikia yule mtu anayeanza kumpongeza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=1d-Z9bnARpk&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 29/05/2020