Pishi ya kinabii hii leo


Swali: Swaa´ ya kinabii inalingana na kiasi gani katika vipimo vya leo?

Jibu: Baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa wamejitahidi kukisia  na wameleta vipimo vya zamani na vya sasa na hawakufikia katika chochote kwa njia ya kukata. Lakini wameafikiana juu ya kwamba ni takriban 3 kg. Fatwa inasema kuwa Swaa´ ya kinabii ni takriban 3 kg.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
  • Imechapishwa: 29/01/2022