Pindi wazazi wanapokukataza kutangamana na watu wema


Swali: Wakiniamrisha wazazi wangu kuachana na marafiki zangu wazuri na wabora na nisisafiri nao kufanya ´Umrah. Je, nalazimika kuwatii katika hali kama hii?

Jibu: Haifai kwako kuwatii katika kumuasi Allaah wala katika mambo yanayodhuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika si vengine utiifu unakuwa katika mema.”

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Anayekuamrisha kutotangamana na watu wema usimtii. Ni mamoja wazazi wawili au wengine. Vilevile usimtii yeyote katika kutangamana na watu waovu. Lakini wazungumzishe wazazi wako kwa maneno mazuri na kwa njia nzuri. Kama vile kusema ´ee baba mpenzi, mambo ni kadhaa… ´, ´ee mama mpenzi, mambo ni kadhaa na kwamba watu hawa ni wema na kwamba unafaidika, moyo wangu unalainika nikiwa pamoja nao, najifunza elimu na nafaidika kutoka kwa watu hao`. Wajibu kwa maneno mazuri, njia nzuri na si kwa ukali na ususuwavu. Wakiendelea kukukataza basi usimwambie kuwa unawafuata watu wema na ni mwenye kuungana nao. Wala usiwaeleze kwamba umeenda pamoja na watu hao ikiwa hawako radhi kwa jambo hilo. Lakini haifai kuwatii isipokuwa katika mema peke yake. Wakikuamrisha kutangamana na watu waovu, wakakuamrisha kuvuta sigara, kunywa pombe, uzinzi au madhambi mengine usiwatii si wao wala wengieno kutokana na Hadiyth mbili zilizotangulia punde kidogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/661)
  • Imechapishwa: 19/02/2021