Pindi utapojua kuwa mwanamke atatumia manukato wakati anapotoka nje


Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kumpa zawadi ya sanduku la manukato mwanamke mwingine pamoja na kuzingatia kwamba mwanamke anayepewa zawadi hutoka kwenda mtaani hali ya kuwa amejitia manukato haya? Je, mtoa zawadi pia anapata dhambi?

Jibu: Hakuna neno kumpa manukato mwanamke. Kwa sababu zawadi inaleta mapenzi na mahaba. Mtoa zawadi anapata thawabu. Mwanamke huyu aliyepewa zawadi akiyatumia manukato haya kwa njia haramu basi dhambi anapata yeye. Lakini ikiwa mtoa zawadi huyu anajua kuwa mwanamke huyu anayetaka kumpa zawadi atayatumia manukato haya katika kutoka kwenda sokoni basi haijuzu kwake kumpa. Kwa sababu hiyo ina maana ya kumsaidia katika dhambi na uadui. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“… na wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”[1]

[1] 05:02

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/42)
  • Imechapishwa: 06/08/2021