Pindi huwezi kuondosha uchafu kutoka kwenye tonge lililoanguka


Swali: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Linapoanguka tonge la mmoja wenu, basi aliondoshe uchafu na alile na wala asimwachie shaytwaan.”[1]

Nifanye nini ikiwa  tonge hilo siwezi kuliondosha uchafu?

Jibu: Ikiwa huwezi kuliondosha uchafu na limechanganyikana na uchafu, hakuna la kufanya. Lakini hata hivyo liweke sehemu ambayo ni safi kwa ajili ya kuitukuza neema.

[1] at-Tirmidhiy (1862).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017