Pigo moja katika Tayammum ni sahihi?


Swali: Nilikuwa safarini na nikafanya Tayammum kwa ajili ya swalah pigo moja tu na kwa mkono mmoja tu. Je, swalah yangu ni sahihi au niirudi tena?

Jibu: Sunnah unatakiwa upige kwa mikono yote miwili. Kilicho salama zaidi katika hili ni wewe kuirudi swalah yako. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfunza ´Imraan akamwabia:

“Upige mikono yako namna hii.”

ambapo akapiga kwa mikono yake juu ya ardhi pigo moja. Ni lazima kupiga kwa mikono yote miwili kisha ufute uso na viganja viwili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2018