Picha zote, mbali na dharurah, ni haramu

Swali: Ni yepi makusudio ya picha ambayo kumekuja makatazo juu yake na kwamba Allaah amewalaani watengeneza picha; picha za vifaa vya kisasa zinaingia katika hayo?

Jibu: Ndio, ule ueneaji unajumuisha picha zote. Ni mamoja ziwe zimetengenezwa kwa vifaa vya kisasa, kwa kuchora, kuchonga n.k. Yote hayo yanaigia katika picha zilizokatazwa. Isipokuwa wakati wa dharurah. Picha wakati wa dharurah hakuna neno. Kuhusu picha kwa ajili ya kutaka tu kujifurahisha au kwa ajili ya sanaa – kama wanavyosema – haifai.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/17421
  • Imechapishwa: 28/12/2017