356 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jibriyl (´alayhis-Salaam) alinijia akasema: ”Nilikuwa nimekujia jana usiku. Hakuna kilichonizuia kuingia ndani ya nyumba uliyokuwemo isipokuwa ni kwamba kulikuwa na kinyago cha sanamu cha mwanamme. Katika nyumba kulikuweko kinyago cha sanamu katika pazia. Amrisha kichwa cha kinyago hicho kikatwe kiwe na umbile kama la mti. Amrisha pazia ikatwe na kufanywe mito miwili inayokanyagwa chini[1]. Amrisha mbwa atolewe nje.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafanya hivo. Mbwa huyo alikuwa ni kilebu cha al-Hasan na al-Husayn kilichokuwa chini ya kitanda chao. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Hakuacha kuendelea kuniusia juu ya jirani mpaka nikafikiri kuwa atamfanya kunirithi.”

Ameipokea Ahmad (2/305) na tamko ni lake, Abu Daawuud (4158), at-Tirmidhiy (2/132) na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” (1487) kupitia kwa Yuunus bin Abiy Ishaaq, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mutme wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Cheni ya wapokezi hii ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim na pia imesahihishwa na at-Tirmidhiy na wengineo…

Mafunzo katika Hadiyth:

4- Maneno yake:

”Amrisha kichwa cha kinyago hicho kikatwe kiwe na umbile kama la mti.”

ni dalili inayojulisha kwamba mabadiliko ambayo yanafanya kufaa kwa picha ni yale mabadiliko yanayoondosha sifa za picha mpaka picha hiyo ikawa na muonekano mwingine kabisa, kama mfano wa mti. Kutokana na hayo haijuzu kutumia picha hata kama ni kwa njia ya kitu kisichoishi. Kwani baadhi ya wanachuoni wako na maoni hayo. Kwa sababu kwa njia kama hiyo bado ni picha kijina na kihakika. Mfano wa picha hizo ni kama zile picha za nusu mtu na mfano wake. Fahamu jambo hili kwa sababu ni miongoni mwa mambo ambayo waislamu wote wanatakiwa wayajue kutokana na kuenea kwa mapicha na kuwa ni jambo la kawaida.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/malaika-hawaingii-maeneo-haya/

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/2/693)
  • Imechapishwa: 30/08/2020