Swali: Unasemaje kumchukua picha mtu kwa nyuma?

Ibn ´Uthaymiyn: Inakuweje?

Muulizaji: Baadhi wanafanya hivo kwa ajili ya kumbukumbu?

Ibn ´Uthaymiyn: Kumbukumbu haiko mgongoni. Utamkumbuka kupitia mgongo wake?

Muulizaji: Baadhi ya wasafiri wanachukua picha hizo kwa ajili ya kumbukumbu.

Ibn ´Uthaymiyn: Ni jambo lisilosilihi. Ni jambo nisiloweze kulifikiria. Unamchukua picha mtu usiyemjua kwa nyuma? Hakuna kitu kama hicho.

Muulizaji: Yanafanyike Shaykh.

Ibn ´Uthaymiyn: Kama yanafanyika basi huo ni upumbavu. Sitoi fatwa yoyote juu ya hilo. Ni upumbavu na si chochote.

Swali: Si chochote?

Jibu: Ni upumbavu. Ni kitu kisichowezekana.

Muulizaji: Kinafanyika Shaykh.

Swali: Mafunzo kwa nyuma? Kwa hali yoyote ni upumbavu. Na kama tukikadiria kuwa kitu hicho kinafanyika basi hakizingatiwi kuwa ni picha. Kitendo hicho ni kama mfano kivuli cha mtu anayetembea juani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (150 B)
  • Imechapishwa: 04/06/2020