Picha – njia inayopelekea katika shirki

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametahadharisha kuvichukua picha viumbe vyenye roho na khaswa kuwachukua picha watu wanaodhimishwa kama vile wanachuoni, wafalme, wachaji, viongozi na maraisi.  Ni mamoja picha hiyo ni kwa njia ya uchoraji kwenye ubao, kwenye karatasi, ukutani, kwenye nguo, kwa njia ya kuchukua picha kwa vifaa vya kisasa vya zama hizi au kwa njia ya kuchonga na kuitengeneza picha kwa sifa ya sanamu. Amekataza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutundika picha kwenye ukuta na mfano wake. Kunaingia vilevile yale masanamu ya ukumbusho. Kwa sababu hiyo ni njia inayopelekea katika shirki. Hakika shirki ya kwanza kujitokeza ulimwenguni ilikuwa ni kwa sababu ya picha na kutengeneza masanamu vinyago. Katika wakati wa Nuuh kulikuweko watu wema. Walipofariki watu wake wakahuzunika ambapo shaytwaan akawashawishi kutengeneza katika vikao vyao walivyokuwa wakikaa masanamu vinyago na wawaite kwa majina yao, jambo ambalo walilifanya lakini hayakuabudiwa. Mpaka walipofari watu wa kipindi kile na elimu ikasahaulika ndipo yakaabudiwa[1].

[1] al-Khattwaabiy ndio ametaja Athar hii katika ”al-Ghunyah ´an al-Kalaam wa Ahlihi”, uk. 22. Lakini asili ya Hadiyth iko katika Swahiyh-ul-Bukhaariy (4636).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 115
  • Imechapishwa: 13/11/2019