Swali: Baadhi ya makampuni wanataka yule mtafutaji kazi aweke picha yake kwenye CV. Inajuzu?

Jibu: Nyinyi mnaelewa fatwa katika masuala haya. Picha wakati wa dharurah inafaa kwa kiasi cha dharurah. Inafaa kwa kiasi cha dharurah peke yake. Ikiwa umelazimika juu ya kazi hii, unaweza kuchukua picha kwa kiasi cha dharurah. Ikiwa unataka kusafiri utalazimika kupiga picha kwa ajili ya pasipoti. Hufanyi hivo kwa sababu ya kupenda picha. Unafanya hivo ili uweze kufikia ile haja yako ya kidharurah. Katika hali hii inajuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (56) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-1-1-1438-01.mp3
  • Imechapishwa: 28/01/2017