Swali: Ni ipi hukumu ya kupiga picha kwa simu kama tunavyoona [msikiti wa] Haram?

Jibu: Haijuzu kupiga picha, si kwa simu, camera, kuchora na kunakili. Picha ni haramu kwa aina zake zote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam) amewalaani watengeneza picha na kueleza kuwa ndio watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah. Aina zote za picha ni haramu. Hili linahusiana na picha za viumbe wenye roho. Ni mamoja iwe katika Haram au kwengine. Ijapokuwa picha Haram ni khatari zaidi. Kwa sababu kufanya maasi Haram ni kubaya zaidi kuliko kufanya maasi nje ya Haram.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13389
  • Imechapishwa: 25/04/2018