Muslim amepokea kutoka kwa Abul-Hayyaaj ambaye ameeleza kwamba ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) alimwambia:

“Hivi nisikutume juu ya kazi aliyonituma kwayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Usiache picha hata moja isipokuwa umeiharibu wala kaburi lililoinuka isipokuwa umelisawazisha.”[1]

Picha imetajwa kwa njia ya kuachia na hivyo inajumuisha picha zote; za kinyago, za kuchora na za kisasa. Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… isipokuwa umeiharibu.”

Picha inaharibiwa kwa kuichanachana. Mtu pia anaweza kuiharibu kwa kukata kichwa chake mpaka kiondoke chote. Picha inakamilika kwa uwepo wa kichwa na uso. Baadhi ya wajinga (au watu wanaotafuta upenyo) wanapiga msitari shingoni mwa picha na inaonekana kama mkufu. Kuharibu hakuwi namna hiyo. Kuharibu kunakuwa ima kwa kukata kichwa au kufuta sifa zake kikamilifu.

[1] Muslim (969).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 607
  • Imechapishwa: 05/09/2019