Picha ambazo Ibn ´Uthaymiyn anajuzisha na anazoharamisha

Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua picha za kumbukumbu sehemu takatifu?

Jibu: Haijuzu kuchukua picha za kumbukumbu kwa watu au wanyama kama ngamia. Haijuzu kwa sababu kitendo hicho kina mapicha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa Malaika hawaingii katika nyumba ilio na mapicha ndani. Isipokuwa tu picha zenye kutweza kama za kwenye magodoro, mito na kadhalika. Kuhusu picha za kumbukumbu za wanyama au watu, hazijuzu kabisa.

Ama picha za kumbukumbu kwa mfano, Ka’bah, mlima wa Minaa, mlima wa ‘Arafah, msikiti Naamirah, msikiti Muzdalifah au msikiti al-Khayr uliyoko Minaa, haina neno maadamu hazipelekei katika kitu cha haramu. Ikiwa picha hizo zitapelekea katika kitu cha haramu nazo zitakuwa ni haramu. Vinginevyo asli ni kuwa zinaruhusiwa.

Swali: Kwenye misikiti hii bila shaka kunakuwepo wanaume, wanawake na viumbe wengine na kuna uwezekano wakaingia ndani ya picha.

Jibu: Ndiyo. Picha ya mtu ikiingia humo basi mtu aondoshe kichwa ili iwe yenye kuruhusiwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (54 B)