Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa pete ya fedha kidoleni?

Jibu: Hakuna ubaya wowote kuvaa pete. Ni mamoja mtu akavaa kuliani au kushotoni. Bora ni kuvaa kwenye kidole kidogo kama alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah.

Kuhusu kuvaa dhahabu haijuzu kwa wanamume. Pete ya dhahabu au cheni ya dhahabu ni kwa wanawake wanaivaa shingoni. Ni kitu kisichofaa kwa wanamume. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewakataza wanaume kuvaa pete ya dhahabu. Wakati alipomuona mwanamume mmoja amevaa pete ya dhahabu akamvua nayo na akaitupa na akasema:

“Atathubutu vipi mmoja wenu kuweka kaa la moto mkononi mwake?”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3975/%D9%85%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%B3%D9%86%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D9%84%D8%A8%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D8%AE%D8%A7%D8%AA%D9%85
  • Imechapishwa: 29/03/2020