Swali: Kuna mtu kafariki na katika dhimma yake ana deni na wala hakuacha mtu wa kumlipia deni lake. Je, deni lake linaweza kulipwa kwa pesa za zakaah?

Jibu: Wametofautiana kwa hili wanazuoni. Na kauli yenye nguvu ni kuwa hakuna ubaya likalipwa na pesa za zakaah. Kwa kuwa mtu huyu ni katika wenye madeni ambao wamo katika fungu la wenye kupewa zakaah kama ilivyokuja katika Aayah. Hivyo ikitolewa zakaah kulipa deni lake, hakuna ubaya – Allaah akitaka – kutokana na kauli yenye nguvu ya wanazuoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid= 8177
  • Imechapishwa: 10/04/2022