Pesa ya kustafu ni haki ya wastaafu

Swali: Nakaribia kustafu kazi. Je, niache kazi na kusamehe haki zangu kwa sababu nimesikia kuwa pesa ya kustafu ina utata?

Jibu: Haina utata – Allaah akitaka. Inatoka katika wizara ya fedha na sio shughuli kati ya watu wawili mpaka mtu aseme kuwa imefanana na ribaa. Pesa ya kustafu ni haki ya huyu mfanyakazi kutoka kwenye wizara ya fedha. Endelea na kazi yako na kisha utaishi kwa kutegemea pesa yako ya kustafu. Nataraji Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ataifanya ni yenye baraka kwako.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58)
  • Imechapishwa: 14/11/2019