Swali: Kundi la kina dada wamekubaliana juu ya kuhifadhi Qur-aan. Wakachanga pesa. Yule ataakayehifadhi kiwango maalum kwa muda maalum basi ndiye atakayechukua pesa hizi. Kwa ajili ya kushaji´isha juu ya kuhifadhi. Je, kitendo hichi kinakubalika katika Shari´ah?
Jibu: Hakuna neno. Huku ni kupeana moyo juu ya kuhifadhi Qur-aan.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
- Imechapishwa: 07/07/2018